ALI KIBA THE SPECIAL ONE

Picha kutoka: Alikiba (facebook)

 Katika wanamuziki ambao huwa hawana kelele kwenye bongo fleva ni Ali Kiba , unaweza sema Ali Kiba hana kitete kulingana na muziki anao ufanya.  Albam ya Only One King imemfanya kuwa tofauti na vijana wachanga ambao wamemkuta kwenye game. Vijana hawa wamekuwa waoga sana hadi kufika hatua kutokuamini Talanta zao na kuamini kuwa kuchafua wengine ni biashara au kutengeneza mahusiano bandia ni muziki jambo ambalo limechangia kuharibu saikolojia ya vijana wengi mtaani na Tanzania kukosa wanamuziki wenye Ubora kama ilivyokuwa awaits.

Miongoni mwa mambo yamechangia Ali Kiba kufanya vizuri bila makelele, majigambo, scandal boland kununua streams au followers kwenye mtandao yake ya kijamii. Ali Kiba anaamini kuwa kazi yake anayoifanya ni nzuri pia anawaamini mashabiki zake, anaamini mashabiki waliompokea mwanzoni ndio hao hao watampambania kufanya vizuri. Ali Kiba anaamini sana katika uzalendo kama ingekuwa hawa wasanii wachanga basi Ali Kiba asingekuwa Tanzania hivi sasa wababa baada tu ya album yake ya Cinderella kufanya vizuri alipata wadhamini wengi sana na kumpa ofa mbalimbali hata kufika kumwambia ahamie chini Marekani watamfanya awe mwanamziki mkubwa kama atakubali kuiacha nchi yake. Ali Kiba alikataa hiyo ofa na kusema kuwa anapenda nchi yake na anapenda awe mwanamziki wa Tanzania. 


Kwa hisani ya Athman Rashid (Ali Kiba The Special One)   (facebook)

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

OSCAR WINNING ACTOR WILLIAM HURT AT AGE 71

Toxic relationships among campus students

Varying meanings of rings on fingers